Ticker

6/recent/ticker-posts

Man United yakamilisha Usajili wa kipa Andre Onana

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya soka ya Uingereza, Manchester United imetangaza kumsajili mlinda mlango wa timu ya taifa ya Cameroon Andre Onana.

Man United walithibitisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Inter Milan ya Italia siku ya Alhamisi kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo.

"Andre Onana amejiunga na Manchester United kwa kandarasi inayoendelea hadi Juni 2028, na chaguo la mwaka zaidi, kibali cha kimataifa kinasubiriwa," taarifa ya Man United siku ya Alhamisi jioni ilisoma.

Klabu hiyo pia ilithibitisha kuwa Onana atavaa jezi namba 24 katika msimu wa 2023/24 unaoanza mwezi ujao.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Cameroon hata hivyo bado hajaripoti katika maskani yake mapya, Old Trafford kwani kuna baadhi ya taratibu ambazo hazijakamilika.

Wakati akizungumza baada ya kuthibitishwa kwa usajili wake katika United, Onana alisema ni heshima kubwa kusajiliwa na klabu hiyo ya EPL na kuweka wazi kwamba anafurahia sana safari yake mpya.

"Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa na nimefanya kazi kwa bidii maisha yangu yote kufikia wakati huu, kushinda vikwazo vingi njiani. Kuenda Old Trafford ili kulinda lengo letu na kuchangia timu itakuwa uzoefu mwingine wa kushangaza. Huu ni mwanzo wa safari mpya kwangu, na wachezaji wenzangu wapya, na matamanio mapya ya kupigania,” alisema.

Aliongeza, "Manchester United ina historia ndefu ya makipa wa ajabu, na sasa nitatoa kila kitu kuunda urithi wangu mwenyewe katika miaka ijayo. Nimefurahishwa na nafasi ya kufanya kazi tena na Erik ten Hag, na siwezi kusubiri kucheza sehemu yangu katika mafanikio ninayojua amedhamiria kutimiza katika klabu hii kubwa ya soka.”

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ni mmoja wa makipa wenye viwango vya juu katika ulimwengu wa soka kwa sasa na amekosa kufungwa katika jumla ya mechi 104 katika mechi 255 alizocheza na klabu.

Hapo awali aliwahi kufanya kazi na kocha wa Man United Erik ten Haag katika Klabu ya Ajax nchini Uholanzi.

Post a Comment

0 Comments