Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Mkuu Yanga (Miguel Gamondi) Afunguka Mazito

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu Wa Yanga Ambaye Ni Mrithi Wa Nabi, afunguka kwamba  Timu Ya Yanga inatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwa sababu ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

Gamondi amesema hayo leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuelekea kilele cha tamasha la siku ya Mwananchi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Kesho ni siku kubwa kwa mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania klabu hii kubwa yenye historia kubwa” amesema Gamondi.

VIDEO: Jezi Mpya za Simba Sc msimu wa 2023/2024

Kocha huyo mpya wa Yanga kutoka Argentina amesema atautumia mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kaizer Chiefs kesho kama sehemu ya maandalizi ya klabu hiyo kwa msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments