Ticker

6/recent/ticker-posts

Usajili Mpya: Willy Eson Onana kutua Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kiungo mshambuliaji wa Rayon Sports ya Rwanda, Willy Eson Onana amekataa baadhi ya ofa alizopewa ili afanikishe dili lake la kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba SC.

Onana ni moja ya wachezaji waliofikia makubaliano mazuri na Simba SC katika kuelekea usajili mkubwa wa msimu ujao utakaofunguliwa hivi karibuni.

Onana mwenye umri wa miaka 23 ndiye kinara wa ufungaji bora katika msimu huu kwenye Ligi Kuu ya Rwanda akifunga mabao 15 huku akipiga asisti 10.

Taarifa imethibitisha kuwa Simba SC imefikia makubaliano mazuri na Onana atakayesaini mkataba wa miaka miwili katika msimu ujao.

Tetesi za usajili Mpya: Simba SC Kusajili kimya kimya

Mmoja wa viongozi wenye ushawishi wa usajili ndani ya Simba SC, amesema kuwa kiungo huyo amefuatwa na baadhi ya timu za ndani ya Rwanda na za nje ikiwemo Singida Big Stars ikihitaji huduma yake.

“Onana amegomea ofa nyingi alizopewa huko Rwanda anapocheza, na kwa hapa nchini alifuatwa na timu baadhi ikiwemo Singida Big Stars.

“Licha ya ofa zote hizo alizopewa, lakini amekataa kusaini na kukubali kuja kujiunga na Simba SC katika msimu ujao baada ya yeye mwenyewe kuonyesha nia kubwa ya kutaka kuichezea Simba SC.

“Tayari taratibu za mwisho za usajili zimekamilika, kilichobakia ni kusaini mkataba pekee wa miaka miwili ambao umeandaliwa tayari,” amesema kiongozi huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amezungumzia hilo kwa kusema: “Tumetenga bajeti kubwa na nzuri itakayofanikisha usajili wa wachezaji wapya ambao tutawasajili katika usajili huu mkubwa utakaofunguliwa.

“Hivyo mashabiki wa Simba SC wajiandae kuwapokea wachezaji wenye ubora na uwezo mkubwa watakaotuvusha katika hatua robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kwenda nusu,” amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments