Ticker

6/recent/ticker-posts

Usajili Mpya: Azam FC kumrudisha Luis Miquissone Tanzania

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Azam FC imedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao,baada ya kukubali kutoa kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh 710.5Mil) kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone raia wa Msumbiji.

Mshambuliaji huyo aliyetolewa kwa mkopo klabu ya Abha inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia akitokea Al Ahly ya Misri hivi karibuni alitajwa kurejea Simba SC kwa ajili ya msimu ujao lakini ikaonekana fedha anayotaka alipwe ni nyingi.

Azam FC wanataka kukamilisha dili hilo la Luis, ikiwa ni saa chache baada ya kumsajili Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutoka Yanga.

Usajili Mpya: Simba Yaweka wazi mipango ya msimu Ujao

Mmoja wa mabosi wa Azam FC, amesema kuwa asilimia hamsini mazungumzo yamekamilika kati ya kiungo huyo na uongozi wa timu hiyo.

Bosi huyo amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha mazungumzo ya mwisho na kiungo huyo kwa kukamilisha dili hilo ambalo atachukua mshahara wa Dola 20,000 (Sh47.3Mil) kwa mwezi.

Ameongeza kuwa muda wowote dili hilo litakamilika na kiungo huyo atajiunga na Azam ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Tunakaribia kuipata saini ya Luis, hivi sasa tupo katika mazungumzo ya mwisho kukamilisha dili hilo la usajili kutoka klabu yake iliyomtoa kwa mkopo Al Ahly.

“Wametupa ofa ya dola 300,000 kama kweli tunamuhitaji mchezaji huyo, ambayo yote hiyo itakwenda kwa mchezaji ni baada ya timu yake kutaka kumtoa kwa mkopo.

“Alitakiwa ajiunge na Simba kwa mkopo, lakini imeshindikana ni baada ya kushindwa kutoa dau hilo la usajili ambalo ni dola 300,000 hivyo kama mambo yakienda sawa, basi tutampa hiyo pesa,” amesema bosi huyo.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ hivi karibuni alizungumzia hilo la usajili kwa kusema kuwa: “Tayari tumemalizana na wachezaji watatu kati ya hao yupo mmoja mzawa, na tutawatambulisha mara baada ya kukamilika kila kitu.”

Post a Comment

0 Comments