Ticker

6/recent/ticker-posts

Maxi Nzengeli kutua Young Africans muda wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Young Africans inaendelea harakati za usajili kwa ajili ya msimu ujao na tayari imemtumia tiketi ya Ndege, winga wa Klabu ya AS Maniema Union ya DR Congo, Maxi Mpia Nzengeli.

Nzengeli ni kati ya wachezaji ambao walikuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Young Africans kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho kwa msimu wa 2023/24.

Winga huyo anayetumia mguu wa kulia, anakuja kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake, Tuisila Kisinda aliyekutana na ‘Thank You’ hivi karibuni akirejeshwa RS Berkane ya nchini Morocco.

VIDEO: Jezi Mpya za Yanga msimu wa 2023/2024

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wenye ushawishi wa usajili, winga huyo jana alianza maandalizi ya safari ya kutoka Kyiv nchini Ukraine kwenda Kinshasa, DR Congo kisha atakuja Dar leo tayari kwa ajili ya kukamilisha dili lake la usajili.

Kiongozi huyo alisema kuwa, winga huyo alitumiwa tiketi hiyo ya ndege baada ya kufikia makubaliano mazuri ya kuja kuichezea Young Africans kwa ajili ya msimu ujao.

Aliongeza kuwa Young Africans haikukutana na ugumu katika kumpata winga, kutokana na yeye mwenyewe kuonyesha nia ya kujiunga na timu hiyo, akivutiwa na baadhi ya wachezaji Wakongo ambao ni Shaaban Djuma, Jesus Moloko, Fiston Mayele na Yannick Bangala.

Leandre Onana atambulishwa Simba SC rasmi

“Maxi hadi jana alikuwa katika maandalizi ya kuanza safari ya kutoka Kyiv kisha ataenda Kinshasa huko DR Congo kuja hapa nchini Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Young Africans.

“Na anakuja kusaini mkataba moja kwa moja, ni baada ya mazungumzo kukamilika kwa asilimia mia moja yaliyofanyika.

“Hivyo mara baada ya kutua nchini, atasaini mkataba wa miaka miwili Young Africans, tunaamini winga huyo anakuja kuwa gumzo hapa nchini kama ilivyokuwa kwa Mayele kutokana na ubora wake,” amesema kiongozi huyo.

Simba SC Yamalizana na Che Fondoh Malone

Meneja wa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe alizungumzia hilo la usajili kwa kusema: “Usajili wa wachezaji wote wapya umekamilika, kilichobakia ni kuwatambulisha pekee na kuanzia wiki hii tutaanza kutambulisha vyuma vipya.”

Post a Comment

0 Comments