Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Soka Barani Ulaya Jumamosi 10.06.2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

West Ham wanavutiwa na dili linalomhusisha mchezaji wa Arsenal Emile Smith Rowe, 22, ikiwa kiungo mwenza wa Uingereza Declan Rice, 24, atajiunga na The Gunners. (Sun)

Ajax wanadai pauni milioni 45 kwa kiungo wao wa kati wa Mexico Edson Alvarez, 25, ambaye ameibuka kama mbadala kwa West Ham kuchukua nafasi ya Rice. (Guardian)

Bayern Munich wanamtaka kiungo wa kati wa klabu ya West Ham Declan Rice lakini wajafanya lolote katika siku za hivi karibuni na Arsenal wanapigiwa upatu kumsajili. (Sky Sport Germany, kwa Kijerumani)

Manchester City wamefanya mazungumzo ya awali na klabu ya RB Leipzig kuhusu usajili wa mlinzi wa Croatia Josko Gvardiol, 21. (Football Insider)

Mazungumzo kati ya Arsenal na Joao Cancelo kuhusu uwezekano wa uhamisho wake yanaendelea vyema na Manchester City wanataka pauni milioni 45 kumnunua beki huyo wa Ureno, 29. (Football Transfers).

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag amezuia majaribio ya Eintracht Frankfurt kumsajili Victor Lindelof msimu huu wa joto, akisema beki huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 28 hawezi kuguswa. (Bild, via Metro).

Chelsea wameanza mazungumzo na Southampton kumhusu kiungo wao wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Football London)

Kipa wa Inter Milan raia wa Cameroon Andre Onana amefikia makubaliano ya kimsingi na Chelsea lakini Inter wamekataa dau la awali la pauni milioni 34 la The Blues kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Tuttomercatoweb, kwa Kiitaliano)

Chelsea pia wanavutiwa na kipa wa AC Milan na Ufaransa Mike Maignan, 27. (L'Equipe, kwa Kifaransa - usajili unahitajika)

Luton Town wamefanya mazungumzo na kipa wa Bosnia Asmir Begovic, 35, ambaye ameondoka Everton - na pia wanamfuatilia mlinda mlango wa Bournemouth wa Jamhuri ya Ireland Mark Travers, 24. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chelsea wanasubiri kuona kama AC Milan watasaini mkataba wa pauni milioni 15 wa kiungo wao Muingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, baada ya kuwatimua wakurugenzi Paolo Maldini na Frederic Massara. (Telegraph - usajili unahitajika)

Klabu ya Saudia Al-Ahli iko tayari kumpa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 32, mkataba wa thamani ya £40m kwa mwaka kuondoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror). 

Tottenham na Manchester United zote ziko tayari kuachana na mpango unaowezekana wa kumnunua David Raya ikiwa Brentford haitapunguza bei yao ya £40m kwa mlinda mlango huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 27. (Standard)

Post a Comment

0 Comments