Ticker

6/recent/ticker-posts

Jonas Mkude Aanza Kazi Yake Rasmi Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Jonas Mkude Kiungo Mpya Wa Yanga, Akiwa Ametokea Ndani ya Kikosi cha Wekundu Wa Msimbazi Ambao ni Watani Wa Jadi Wa Klabu Yake Hiyo Mpya Ya Yanga, ameanza kazi yake kuelekea msimu mpya wa 2023/24.

Mkude mzawa mwenye uwezo eneo la kiungo atakuwa na uzi wa Yanga baada ya Kuondoka Simba Akiwa Huru 

Nyota huyo alipewa mkono wa asante na Simba timu ambayo amecheza kwa muda wa miaka 13 kwenye soka la ushindani na kujiunga na Yanga.

PICHA: Young Africans Wakijiandaa na Wiki ya Mwananchi

Simba ilipompa mkono wa asante akapata dili kwa watani wa jadi Yanga hivyo bado yupo mitaa ya Kariakoo Mkude.

Tayari timu ya Yanga imeanza maandalizi ikiwa imeweka kambi Kigamboni kuelekea msimu mpya.

Julai 22 ni Wiki ya Mwannachi na Yanga natarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs.

Katika mazoezi yao kiungo Bernard Morrison ambaye naye kwa sasa ni Mchezaji  huru baada ya kupewa mkono wa asante aliwatembelea kwenye mazoezi hayo.

Post a Comment

0 Comments