Ticker

6/recent/ticker-posts

VIDEO: Jezi Mpya za Simba Sc msimu wa 2023/2024

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Simba Sc tayari imefanikiwa kutambulisha jezi zake mpya za msimu wa 2023/24 zikiwa na majina ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar Jezi hizo zimezinduliwa hii leo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Moja ya viongozi majina yao yaliyopo kwenye jezi ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais, Philip Mipango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

Jezi yenye rangi nyekundu ndio jezi pekee iliyopelekwa Mlima Kilimanjaro ikiwa na jina la mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji.

Jezi ipi imekuvutia zaidi?

 Unawapa Asilimia Ngapi Simba kwa Uzi huu?

Post a Comment

0 Comments