Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba SC yamrejesha Luis Miquissone Rasmi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Hatimaye Klabu ya Simba SC Imefanikiwa kumrejesha Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone  kama mchezaji huru, baada ya kufanikiwa kuvunja mkataba na Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya Misri.

Miquissone aliondoka Simba SC miaka miwili iliyopita akisajili Al Ahly, baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, akiifunga bao pakee na la ushindi katika mchezo wa Mzunguuko wa pili hatua ya Makundi msimu wa 2020/21.

VIDEO: Jezi Mpya za Simba Sc msimu wa 2023/2024

Simba SC imemtambulisha rasmi mchezaji huyo kupitia vyanzo vyake vya habari, ikiwa ni tukio la kwanza kutangazwa baada ya kutambulishwa kwa jezi za msimu mpya za klabu hiyo jana Ijumaa (Julai 21) majira ya saa moja usiku.

Kurejea kwa Miquissone ni faida kubwa kwa simba sc kwani tayari ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika lakini kubwa zaidi analijua vema soka la Tanzania.

Tayari Miquissone ameshawasili Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda Uturuki

Miquissone anataraji kuondoka mapema wiki ijao kuelekea Uturuki ambapo atajiunga na wenzie kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/2024

Ujumbe alioambatana na picha ya utambulishi wa Miquissone katika vyanzo vya habari vya Simba SC umeandikwa: Amerudi anapostahili kuwepo. Karibu tena nyumbani, Luis Miquissone. #NguvuMoja

VIDEO
 Luis Miquissone AKITAMBULISHWA

Post a Comment

0 Comments