Ticker

6/recent/ticker-posts

Erik Ten Hag Avutiwa na Marco Reus

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anavutiwa na kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus na wiki iliyopita kocha huyo alikutana na wawakilishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani.


Wakala wa Marco Reus, Dirk Hebel na Darren Freeman, walionekana Old Trafford wakitazama mchezo kati ya Manchester United na Manchester City.


Reus, 33, amebakiza miezi sita katika mkataba wake na Borussia Dortmund. Ametumia miaka 11 katika klabu hiyo tangu aliposajiliwa kutoka Borussia Mönchengladbach mwaka 2012.


Kwa mujibu wa Christian Falk kupitia mtandao wa Caught Offside, klabu hiyo inafikiria kumnunua mkongwe huyo wa Bundesliga.


Falk, ambaye ni mwandishi mkuu wa habari za michezo katika jarida la Ujerumani la Bild, alisema kuwa Ten Hag alikutana na Hebel na Freeman kujadiliana kuhusu Reus, hali ya mkataba wake, na uwezekano wa kuhamia United majira ya kiangazi.


Kwa sasa Dortmund wana nia ya kupunguza kwa kiasi kikubwa mshahara wa €200,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.


Mawakala wa Reus pia wamekutana na Uongozi wa klabu mpya ya Cristiano Ronaldo, Al-Nassr Kujadili uwezekano wa Mchezaji huyo kujiunga nao.


Tofauti na Dortmund, kwa upande wa  Al-Nassr wao wapo tayari kuboresha kwa kiasi kikubwa mshahara wa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani.


Ten Hag anamtaka Reus kuhudumu kama mbadara wa Bruno Fernandes. 


Memphis Depay Atua Atletico Madrid Akitokea BarcelonaPost a Comment

0 Comments