Ticker

6/recent/ticker-posts

Memphis Depay Atua Atletico Madrid Akitokea Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Atletico Madrid wamemsajili fowadi mzoefu raia wa Uholanzi, Memphis Depay, 28, kwa kitita cha Euro milioni 3 kutoka Barcelona.


Depay ambaye mkataba wake na Barcelona ulitarajiwa kutamatika mwishoni mwa msimu huu wa 2022-23, ametia saini kandarasi ya miaka miwili na nusu katika kikosi cha Atletico ambacho pia kinashiriki Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).


Kwa mujibu wa makubaliano, Barcelona sasa wako huru kumsajili fowadi Yannick Carrasco raia wa Ubelgiji, kutoka Atletico wakati wowote.


Depay ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester United, amechezea Barcelona mara nne pekee katika kampeni za msimu huu baada ya kutatizwa pakubwa na jeraha la paja.


Alihamia kambini mwa Barcelona bila ada yoyote mwanzoni mwa msimu wa 2020-21 baada ya kuagana na kikosi cha Olympique Lyon cha Ufaransa na akapachika wavuni mabao 14 kutokana na mechi 42.


Atletico walilazimika kumsajili Depay baada ya kukatiza uhusiano na fowadi Joao Felix aliyejiunga na Chelsea kwa mkopo wa msimu mmoja mwanzoni mwa Januari 2023.


De Gea Akasirika Baada Ya Casemiro Kupigwa Marufuku Kucheza Dhidi Ya Arsenal


Post a Comment

0 Comments