Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Sc kuwakabili KMC CCM Kirumba, Mwanza

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

SIMBA SC inashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kuwakabili wenyeji KMC katika Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC leo saa Kumi jioni.


Simba inashuka katika mchezo huo ikiwa Imeambulia sare ya tano msimu huu baada ya kutoka nyuma na kuibana Kagera na kufanikiwa kutoka sare ya goli 1-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba siku ya Jumatano.


Hadi sasa Simba Sc wapo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 38 baada ya Azam kukubali kipigo cha Mabao 3-2 kutoka kwa Yanga katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.


Kocha mkuu wa muda wa timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Juma Mgunda ana majeruhi na hatapata huduma ya mshambuliaji Mzambia Moses Phiri. Phiri, ndiye mfungaji bora wa klabu hiyo mbaka sasa akiwa na mabao kumi ya ligi, baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar kitu ambacho kinaweza kumuweka nnje hadi katikati ya mwezi ujao.


Siku ya Jumamosi, Simba ilithibitisha kumsajili Said Ntibazonkiza kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Burundi anaweza kucheza dhidi ya KMC.


Mbaka sasa Ntibazonkiza ana mabao manne na asisti sita katika mechi 12 za ligi,  hivyo anaenda kuongeza kitu kwenye kikosi cha Simba.


Kukosekana kwa Phiri, Kuna mlazimu Kocha Juma Mgunda kumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Yanga katika mchezo wa simba dhidi ya KMC.


Mgunda pia atakuwa na viungo Victor Akpan na Jonas Mkude baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu. Wote wawili walikuwa kwenye benchi katika safari yao ya Kanda ya Ziwa wiki iliyopita.


Pia kiungo Peter Banda sasa yuko fiti baada ya kukosekana tangu mwanzoni mwa Novemba kutokana na tatizo la misuli ya paja.


Kwa upande wa wenyeji KMC, baada ya kufanya vibaya katika michezo yake ya mwezi Septemba na Oktoba, inaonekana kwamba siku za kocha mkuu Thierry Hitimana zinahesabika ndani ya klabu hiyo.


Ingawa KMC imekuwa na mwazo mzuri mwezi huu, walianza mwezi kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya, kisha wakatoka sare ya kutofungana na Prisons.


Walirejea katika fomu ya ushindi kwa ushindi mnono dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania.


Wamepanda hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC - wakiwa pointi tano mbele ya eneo la kushushwa daraja na pointi tatu tu kutoka nafasi ya tano bora.


Sasa wameimarisha tofauti yao ya mabao, kwa kufunga mabao mengi zaidi ya waliyofungwa.


Mchezo safi wa hivi karibuni dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union umechangia suala hilo kwa kiasi kikubwa.


Kocha Hitimana Atawakosa wachezaji Matheo Anthony au Hance Masoud katika mchezo huo. Hivyo, itambidi kuchagua wachezaji wengine kutoka kwenye kikosi hicho.


Kwa takwimu, Simba na KMC zimekutana katika mechi tisa za ligi tangu msimu wa 2018/19.


Simba imeshinda mechi nane na kutoka sare ya 2-2 mwezi Agosti kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Yanga Yambakisha Dickson Job, Apewa Mkataba MnonoPost a Comment

0 Comments