Ticker

6/recent/ticker-posts

Augustine Okraha kuanza kazi leo Young Africans

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Gamondi, amefichua kuwa winga mpya wa timu hiyo, Augustine Okraha ataonekana uwanjani katika mechi mbili zijazo za Kombe la Mapinduzi.

Benchikha abadili mipango ya usajili Simba SC

Okrah amejiunga na Young Africans kwenye usajili wa Dirisha Dogo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Bechem United ya Ghana, alitambulishwa juzi Jumapili (Desemba 31) kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, wakati Young Africans ikicheza mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri.

Winga huyo ambaye aliwahi kuitumikia Simba SC msimu uliopita, alifanya vizuri aliporejea Ghana kuichezea Bechem United ambapo katika mechi 15 za Ligi Kuu msimu huu, alifunga mabao 9.

Leonel Ateba kutua Young Africans

Akizungumzia usajili wa Okrah, Gamondi alisema: “Leo Jumanne pengine anaweza kucheza kwa sababu kifiziki yupo vizuri au mchezo wa mwisho.”

Post a Comment

0 Comments