Ticker

6/recent/ticker-posts

Ligi Kuu ya NBC: YANGA SC 3-2 AZAM FC

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU ya Yanga Sc imezidi kujiimarisha katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufanikiwa kuibuka na Ushidi wa mabao 3-2 dhidi Azam FC uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.


Katika mchezo hou Yanga ilicheza bila kiungo wake tegemeo FAISAL SALUM "Fei Toto" anayedaiwa kusajiliwa na Azam FC.


Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abdul Sopu dakika ya 27 akimalizia pasi safi ya Prince Dube huku Yanga wakipata mabao yao kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 31 na Stephane Aziz Ki dakika ya 33 na kwenda mapumziko Yanga wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-1.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Azam FC kufanikiwa kupata bao la mapema dakika ya 47 likifungwa tena na Abdul Sopu likiwa ni goli lake la 5 dhidi ya kipa Djigui Diarra huku bao la ushindi la Yanga SC likifungwa na Farid Mussa dakika ya 78 baada ya kiungo Stephane Aziz Ki kupiga shuti lililo mshida golikipa wa Azam na kumkuta Farid Mussa.


Kwa ushindi huo Yanga SC wamefikisha Pointi 47 na kuiacha Azam FC kwa tofauti ya Pointi 10 huku Simba wakiachwa kwa pointi 9 kabla ya mchezo wa leo dhidi ya KMC katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Simba Sc kuwakabili KMC CCM Kirumba, Mwanza


Post a Comment

0 Comments