Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Usajili Wa Miquissone, Manzoki

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

KLABU ya Simba imetoa ufafanuzi kuhusu usajili wa wachezaji Luis Miquissone na Cesar Manzoki katika kipindi hiki cha dirisha dogo na kusema watakapo kamilisha mchakato huo watawatangazia mashabiki wao.


Miquissone anakipiga katika klabu ya Al Ahly ya Misri ambayo inahitaji kumtoa kwa mkopo na Manzoki anacheza DL Pro inayoshiriki Ligi Kuu ya China, wanahusishwa zaidi na Simba katika usajili huu wa dirisha dogo tangu lilipofunguliwa.


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema wanafanya usajili mzuri na wanaenda kununua mikataba ya wachezaji wakubwa ambao wanawahitaji.


Alisema kuhusu Miquissone na Manzoki ni wachezaji wazuri na kulingana na uwezo wao hakuna timu isiyohitaji huduma za nyota hao ila wanaheshimu mikataba yao.


"Hao wachezaji wana mikataba na klabu zao, tunaheshimu sana na kama itakuwa wako katika mipango yetu basi tutalazimika kufanya nao mazungumzo na hizo klabu ila kwa sasa tunaheshimu mikataba yao," alisema Ahmed.


Aliongeza mapendekezo waliyopokea kutoka katika benchi la ufundi lililoko chini ya Juma Mgunda, watayafanyia kazi kwa kuwanasa wote wanaolengwa iwe kwa kutumia dau kubwa au kuvunja mikataba waliyokuwa nayo.


SOMA HAPA KUHUSU: Kocha Mpya Simba Huyu Hapa....Kuja Na Cesar Manzoki


Post a Comment

0 Comments