Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Mpya Simba Huyu Hapa....Kuja Na Cesar Manzoki

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

SIMBA inatarajia kumtambulisha raia wa Brazil Robert Oliveira ‘Robertinho’ kama kocha wao Mpya baada ya kocha huyo  kuvunja mkataba na timu yake ya Vipers ya nchini Uganda kwa makubaliano ya pande zote mbili.


Klabu Vipers imetangaza kupitia akaunti rasmi ya klabu hiyo kwamba Oliveira anaondoka kwenye timu hiyo kama Kocha Mkuu na watatangaza mbadala wake.


“Klabu inapenda kumshukuru Robertinho kwa juhudi zake alipokuwa Kocha Mkuu, wakati alipokuwa klabuni hapa na tunamtakia mafanikio mema katika siku zijazo, ” ilieleza taarifa hiyo.


Vipers imeeleza kuwa ndani ya muda mfupi iwezekanavyo itatoka na taarifa kuhusu uongozi wa benchi la ufundi kufuatia kuondoka kwa kocha huyo.


Hata hivyo sababu za Kocha huyo kuondoka Vipers SC hazijaelezwa, zaidi ya kuwepo kwa tetesi huenda akawa amepata kazi mahala kwingine, ambako amepata dili nono zaidi.


Tayari Uongozi wa Simba SC kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amethibisha kuwa, Klabu yao ipo mbioni kumleta Kocha Mkuu mpya, ambaye atasaidizna na Kocha Juma Mgunda ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya Kocha Mkuu.


Pai taarifa za kina tulizozipata kutoka ndani ya klabu ya simba ni kuwa kocha huyo ataungana na mshambuliaji wake wa zamani CESAR MANZOKI aliye mfundisha wakati akiwa Vipers ya nchini Uganda.

Post a Comment

0 Comments