Ticker

6/recent/ticker-posts

Dodoma Jiji Yataka Wawili Kutoka Yanga Sc

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Klabu ya Dodoma Jiji imejitosa kuwani Saini za Wachezaji Heritier Makambo na Yusuf Athuman wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.


Mpango huo umefahamika kufuatia wawili hao kuwa sehemu ya wachezaji watakao tolewa kwa Mkopo, huku Klabu nyingine inayotajwa kuwawania ni Coastal Union ya jijini Tanga.


Hata hivyo Dodoma Jiji FC inadaiwa kuweka nguvu zaidi kwa Mshambuliaji mzawa Yusuf Athumani kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji, wakiamini hata Mshambuliaji huyo atawatosha, endapo watashindwa kuwanasa wote wawili.


Kwa sasa kikosi cha Klabu hiyo ya Jijini Dodoma safu yake ya ushambuliaji inataabika licha ya kuwa na majembe ya maana akiwamo, Collins Opare, Zidane Sereri, Hassan Mwaterema, Paul Peter na Christian Zigah.


Nyota hao bado hawajamkuna Kocha Mellis Medo na sasa Raia huyo wa Marekani anataka kuongeza nguvu katika safu hiyo na kati ya walio kwenye rada zao ni nahodha wa Geita Gold, Danny Lyanga na Yusuf Athuman.


Yusuf alisajiliwa Yanga SC misimu miwili iliyopita akitokea Biashara United Mara, na amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Mabingwa Soka Tanzania Bara.


Mmoja ya viongozi wa Dodoma, Fredrick Mwakisambwe amesema Ripoti ya benchi la ufundi inahitaji mshambuliaji, kiungo na beki mkabaji, huku akikwepa taarifa za Yusuf wenyewe wakiamua kufanya siri.

Post a Comment

0 Comments