Ticker

6/recent/ticker-posts

Rasmi! Ronaldo Ajiunga Na Al Nassr Ya Saudia Arabia Kwa Mkataba Wa Kuvutia Wa Pauni Milioni 175 Kwa Mwaka

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia imedhibitisha kuinasa saini ya nyota wa Ureno Christiano Ronaldo.


Al Nassr wamedhibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wao wa Instagram ambapo rais wa timu hiyo alionekana ameshika jezi pamoja na Ronaldo na kusema kuwa kuzipata huduma zake ni zaidi ya historia ambayo klabu hiyo imeandikisha.


“Hii ni zaidi ya historia katika utengenezaji. Huu ni usajili ambao sio tu utaipa klabu yetu msukumo wa kupata mafanikio makubwa zaidi bali utaipa msukumo ligi yetu, taifa letu na vizazi vijavyo, wavulana na wasichana kuwa toleo bora zaidi lao. Karibu @cristiano kwenye familia yako mpya @alnassr_fc” Waliandika kwenye Instagram.


Ronaldo alithibitisha kuhamia kwa timu hiyo ya Saudi Arabia kwa mkataba wa kuvutia wa pauni milioni 175 kwa mwaka baada ya kuondoka kwa misukosuko kutoka Manchester United mwezi Novemba.


Ronaldo, mwenye umri wa miaka 37, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka United baada ya mahojiano yake na Piers Morgan ambayo yalisumbua na ya kutatanisha, huku mashabiki sasa wakimiminika kwenye mitandao ya kijamii kudai kuwa 'ameisha' baada ya kuhamia Mashariki ya Kati.


Ripoti nchini Saudi Arabia zinaeleza kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili.


Imedaiwa kuwa sehemu ya jukumu lake kama balozi ni kuisaidia Saudi Arabia katika ombi la pamoja na Misri na Ugiriki kuandaa Kombe la Dunia la 2030.


YAFAHAMU MAISHA YA PELE NJE YA UWANJA


Post a Comment

0 Comments