Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba, Yanga zaanza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Ushindi mnono Ugenini

WAWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa Afrika) Simba na Yanga wameanza kampeni zao katika Ligi hiyo kwa kupata ushindi mnono Ugenini.

Yanga imeichapa bila huruma Zalan FC ya Sudan Kusini mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku Simba ikiichapa Nyasa Big Bullets mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu mjini Lilongwe, Malawi.

Kwa upande wa Yanga, mshambuliaji Fiston Mayele ameingia kwenye rekodi baada ya kupachika hat-trick huku Feisal Salum akichangia bao moja na kuiwezesha timu hiyo kuibuka washindi mnono.

Nchini Malawi, Simba imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji Moses Phiri na mchezaji wa akiba John Bocco aliyefunga Simba goli la pili dakika za mwisho za mchezo na kufanya Wekundu hao kuondoka na Ushindi Ugenini.

Hata hivyo, wawakilishi hao watacheza mechi ya marudiano wikendi ijayo huku Simba wakiwakaribisha Wamalawi katika uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.

Pia, Yanga watakuwa kwenye uwanja huo wakiwakaribisha Zalan FC ambao watakuwa katika hali ya kupambana na kusaka kupindua matokeo ya mabao 4-0 na kutinga hatua inayofuata.

Kesho, itakuwa zamu ya Geita Gold kuanza kampeni hiyo kwa kuminyana na Hilal Alsahil ya nchini Sudan.

Post a Comment

0 Comments