Ticker

6/recent/ticker-posts

Shomary Kapombe Atangaza Vita Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BEKI wa Simba, Shomary Kapombe amesema msimu uliopita ulikuwa mgumu kwa upande wao na kutangaza vita kwa msimu ujao akisema wanajipanga kuhakikisha wanarejea na moto na kuwapa furaha ya mashabiki wa klabu hiyo.


Msimu uliopita, Simba ilipoteza mataji matatu la Ligi Kuu, Kombe la ASFC na Ngao ya Jamii yote yakichukuliwa na watani wao, Yanga.

Kwa mujibu wa Kapombe wanajipanga kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza mpaka kusababisha kumaliza ligi kinyonge.

“Msimu huu kwetu haukuwa mzuri, tumepoteza kila taji jambo ambalo hata sisi wachezaji limetuuma sana, sio mashabiki pekee walioumizwa,” alisema Kapombe ambaye ni mchezaji wa zamani wa Ashanti United na Azam. Aidha Kapombe amewataka mashabiki wao kuendelea kuwasapoti watakapoanza msimu ili waweze kufanya vizuri kwa kuwa sapoti yao inahitajika katika mafanikio ambayo Simba imeyapata.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye yuko nje ya nchi kwa sasa, alisema uongozi walishabaini mapungufu yaliyopo mpaka kupoteza mataji hayo, wanayafanyia kazi kuelekea msimu ujao.

“Ndio matokeo ya mpira yalivyo, msimu ujao naamini tutarejesha heshima yetu tuliyoitengeneza miaka minne mfululizo, wanasimba wawe na imani na viongozi wao,”alisema Try Again.

Kikosi cha klabu hiyo kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea nchini Misri katika mji wa Ismailia kwa ajili ya kambi kujiandaa na msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments