Ticker

6/recent/ticker-posts

TETESI ZA USAJILI MPYA SIMBA SC NA ISHU YA NTIBAZONKIZA....….

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BAADA ya kukosa mataji mabosi wa Simba SC, wameamua kuingia sokoni kupambana kwa hali na mali ili kukiongezea nguvu kikosi hicho ili kurudisha ubingwa waliyopoteza msimu uliopita kwa watani wao Yanga.


Msimu huu walianza kwa kupoteza Ngao ya Jamii baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Yanga, ni mataji mawili yamebaki wakiyawania kwa sasa. Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Ligi Kuu Bara. Pia wapo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, amebainisha mipango Ya timu hiyo kwa msimu huu namna hii.


“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi tunazocheza na ukizingatia kwamba kila timu inapambana kupata matokeo mazuri uwanjani.


“Hata sisi tunapambana pia kwani huwezi kupata pointi kwenye mchezo, kamahakutakuwa na mipango makini, hivyo kazi ipo na inaendelea.


Mzunguko wa pili hesabu zipoje?


“Kwenye mzunguko wa kwanza ambao umepita tulikuwa imara lakini sio kwa kiwango kikubwa tulichokuwa tunakitaka.


“Kuna mechi ambazo tulishindwa kupata ushindi na tulipoteza, hayo ninaamini kwamba benchi la ufundi limeona na limefanyia kazi, hivyo kwa mzunguko wa pili kutakuwa na tofauti kwenye kila mchezo.


“Mechi za ugenini zilikuwa ni ngumu na zitazidi kuwa ngumu lakini ambacho tutakifanya ni kupambana kupata pointi, huwezi kushinda ubingwa ikiwa utakuwa unashindwa kupata pointi.


Wapinzani wenu mnawatazamaje?


“Ni wapinzani wanaoleta ushindani, unaona Geita Gold wakiwa nyumbani huwa wanatupa ushindani kama ilivyokuwa msimu uliopita tulishindwa kupata alama tatu kwao lakini safari hii mpango umekuwa tofauti.



Wakati wa dirisha dogo maeneo yapi mtafanya maboresho?


“Ukianza na safu ya ushambuliaji, ukweli ni kwamba tuna safu imara ambayo inafunga mabao mengi, lakini tuna mashindano mengi ya kitaifa na kimataifa, hapo lazima uwe na watu wa kazi kwelikweli.


“Tunahitaji kuboresha kwenye eneo la ushambuliaji kwa kuongeza watu wa kazi na hapo tunaamini tukikamilisha tutatoa taarifa kamili.


“Pia kwenye safu ya ulinzi ni lazima tufanye maboresho eneo hilo ili kuwa na uhakika wa kile ambacho tutakifanya kwenye ushambuliaji kitakuwa kinalindwa na mabeki imara.


“Haina maana kwamba hawa tulionao hawana uwezo, hapana, wana uwezo mkubwa na ndio maana tumefungwa mabao machache kwenye ligi, tunataka uwepo mwendelezo zaidi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza.


Kimataifa hesabu zipoje?


“Huko ni lazima tuwe na hesabu kubwa na ngumu ukizingatia kwamba kila timu ambazo tunakutana nazo zimejipanga kufanya vizuri.


“Kukutana na mabingwa kwenye mechi za kimataifa ni muhimu kuwa na mipango itakayoleta matokeo mazuri na ukizingatia kwamba tunawakilisha Tanzania kwenye haya mashindano.


“Wachezaji ambao tupo nao ikiwa ni pamoja na Moses Phiri, Clatous Chama, John Bocco ni moja ya wachezaji wenye uzoefu na kila mmoja anatambua majukumu yake.


Vipi kuhusu Saidi Ntibazonkiza?

“Ntibazonkiza ni moja ya wachezaji wazuri hasa kutokana na uzoefu alionao anakupa mengi, anajua kupiga pasi za mabao, anajua kufunga na anaweza kupiga mipira iliyokufa.


“Tunajua kwamba ni mali ya Geita Gold, hivyo ni suala la kusubiri na kuona kwani tukimpata tutakuwa tumelamba dume,” anasema Ally.


Sadio Ntibanzokinza atua Simba Sc



Post a Comment

0 Comments