Ticker

6/recent/ticker-posts

Nasreddine Nabi: Nina sapraizi mbili

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ana sapraizi mbili za kumalizia usajili kwenye benchi lake la ufundi. Anataka mtaalam wa kusoma video za wapinzani ambao ni wazi kwamba wataanza na Simba kwenye mechi ya ngao ya jamii Agosti 13. Pia anamshusha mtu wa lishe kama zinavyofanya klabu kubwa za Ulaya.

Nabi alisema waliopo sasa atabaki nao, kuanzia msaidizi wake wa kwanza Cedric Kaze na mpaka mtu wa mwisho lakini bado anataka watu zaidi wa maana ambao hao ndio funga kazi.


Kocha huyo bora wa msimu uliopita akiwapa Yanga mataji matatu anataka kuongeza wataalamu zaidi katika benchi lake wakiwemo wataalam wa kuchambua mikanda ya wapinzani lengo kubwa ikiwa ni kufanya kitu tofauti CAF.

“Hawa wasaidizi wangu wote niliokuwa nao nimewaambia viongozi nimeridhika na ufanisi wao, kuanzia Kaze (Cedric) na wote wengine waliosalia nataka kuendelea nao,”alisema Nabi ambaye mtihani wake wa kwanza msimu ujao ni kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambako amepania kwa namna yoyote ile kufika mbali.

“Kuna watu zaidi tutawaongeza hapa kama uongozi utafanyia kazi kwa ufanisi, ukiangalia sasa sisi makocha ndio tumekuwa tukitafuta mikanda ya wapinzani na kuifanyia kazi.

“Tunahaja ya kuwa na mtu maalum wa kufanya hii kazi ambaye ana ubora kisha akaimaliza ataleta ripoti kwetu na sisi tunakwenda kufanyia kazi, tunakwenda kwenye mashindano magumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika lazima uwe na mbinu za kisasa,”alisema.

Nabi aliongeza kuwa mbali na mtaalam huyo pia anataka kuwa na mtaalamu wa lishe ambaye atasimamia mfumo mzima wa lishwe wa timu hiyo.

“Mpishi wa chakula hapa lakini tunahitaji pia mtu wa lishe aliyesomea taaluma ya lishe kwa wachezaji ili tuweze kuwa salama zaidi eneo hilo.”


AWAPIGIA SIMU MASTAA

“Morrison (Bernard) alishapewa programu ya mazoezi na inafuatiliwa kwa karibu. Nilianza kuzungumza na Kambole (Lazarous) nimemkaribisha hapa na najua sasa mambo mengi na nimemwambia ninachotaka.

“Nimeongea pia na Lomalisa (Joyce) bado sijaongea na Bigirimana na Azizi KI, hawa ni watu wapya lazima uongee nao kwa kuwapa heshima lakini pia wajue wanatakiwa kufanya nini kuanzia muda huu mpaka wakati watakapojiunga na timu.

“Nimewaambia viongozi ilikuwa Aziz KI aje mapema lakini kuna shida ya usafiri wa kuunganisha kutoka nchini kwao tumekubaliana kwamba akifika aje moja kwa moja ili kuokoa muda asije kuchelewa kuanza maandalizi, hatuhitaji kuacha mtu nyuma.” Nini maoni yako kuhusu Yanga mpya. Tuma meseji kwenye namba hapo chini.

Post a Comment

0 Comments