Ticker

6/recent/ticker-posts

Barcelona wamtaka Frenkie de Jong kujiunga Man Utd

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Barcelona wamtaka Frenkie de Jong kukubali Ofa ya Man Utd


Barcelona wamemwambia kiungo wao Frenkie de Jong kuondoka klabuni hapo, Barca imemjulisha mchezaji huyo kwamba lazima akubali ofa ya Manchester United.


Barca wamekubali ofa kutoka kwa Manchester United siku ya Alhamisi - Ambapo €75m ni ada ya uhamisho na nyongeza ya €10m.


Baada ya Ada hiyo kukubaliwa, kilichobaki kukamilisha uhamisho huo ni De Jong kukubali kusaini mkataba na Mashetani Wekundu, Barca wanamshawishi sana kiungo huyo kukubali.


Barca inasemekana wamempa sharti moja tu De Jong ni yeye kukubali ofa ya Man Utd la sivyo, wapo tayari kumuacha kiungo huyo katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya Amerika Kaskazini iwapo atakataa kuondoka.


Klabu hiyo pia imeonekana kumpa Ferran Torres jezi namba 21 iliyokuwa ikivaliwa na De Jong-ingawa mabadiliko hayo bado hayajatangazwa na klabu hadi sasa. 


De Jong ameonyesha nia ya kuungana tena na meneja wake wa zamani Erik ten Hag, huku vyombo vya habari jijini Catalunya vikiripoti kuwa ni ngumu Barca kukataa ofa hiyo ya Man Utd .


Ni wazi kwamba Barca wanamuondoa  De Jong msimu huu wa majira ya joto ili kupisha wachezaji wapya Franck Kessie na Andreas Christensen - ambao wote walitambulishwa kama wachezaji wa Barca wiki iliyopita ambao bado hawajasajiliwa kwa sababu ya sheria za usawa wa kifedha kwa vilabu vya La Liga.

Post a Comment

0 Comments