Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele Amkaribisha Bernard Morrison Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mayele Amkaribisha Bernard Morrison Yanga 

Straika wa Klabu ya Yanga ambaye ni raia wa Congo DR, Fiston Kalala Mayele amemkaribisha aliyekuwa staa wa Simba Sc, Bernard Morrison katika familia ya Yanga ili kuitumikia klabu hiyo.

Mayele kupitia ukurasa wake wa Twitter, ameposti picha ya Mayele na kuandika maneno haya "Name the Player in EPL terms?" akimaanisha "Mtaje mchezaji huyu kwa vigezo vya EPL (Ligi Kuu ya Uingereza)?"

Usiku wa kuamkia leo, Klabu ya Yanga imemtangaza Morrison ambaye ni raia wa Ghana kuwa mchezaji wake akitokea kwa mahasimu wao wa jadi, Simba Sc ambako amemaliza mkataba wake.

Soma Pia | Pape Ousmane Sakho Azidi Kung'ara Simba

Ikumbukwe kuwa, Morrison amewahi kucheza Yanga, nusu msimu wa mwaka 2019/2020 kabla ya kutimkia Simba ambako ameitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili na kisha sasa anarejea tena Yanga.

Hivi karibuni kumekuwepo na stories nyingi kuhusu Morrsion kushindwana na Simba huku yeye akifunguka kuwa katika mkataba wake mpya walimpunguzia mshahara jambo ambalo hakukubaliana nalo hivyo ameamua kuondoka.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Post a Comment

0 Comments