Ticker

6/recent/ticker-posts

Pape Ousmane Sakho Azidi Kung'ara Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Pape Ousmane Sakho Azidi Kung'ara Simba

Pape Ousmane Sakho au Mzee wa Kunyunyiza; ni mchezaji wa Simba katika nafasi ya kiungo wa kisasa mwenye uchezaji mzuri wa mpira, ujuzi na haraka ambaye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Sakho, raia wa Senegal amewapiku wakali wenzake wawili, Peter Banda na Kibu Dennis ambao pia walikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Sakho amepata jumla ya kura 445 sawa na asilimia 58.71 akifuatiwa na Banda aliyepata kura 234 (30.87%) huku Kibu akipata kura 79 sawa na asilimia 10.42. 

Katika mwezi Juni, Sakho amecheza mechi tatu kati ya tano sawa na dakika 221 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana mawili.

Sakho amekabidhiwa tuzo na fedha taslimu sh. Mil 2 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Sakho kunyakua tuzo hiyo, aliwahi kuipata mapema Januari mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments