Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipa KMC Faruk Shikhalo Afunguka!

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kipa KMC Faruk Shikhalo Afunguka  amejishtukia kwa kusema malengo yake kwa msimu huu yametimia, ila kwa sasa anajipanga ili kuboresha zaidi kwa msimu ujao.

Shikhalo aliyemaliza mkataba wake na KMC msimu uliomalizika amewahi kung’ara na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Kenya alikokuwa akiidakia Bandari FC ya Kenya.

Akizungumza Jijini hapa, Shikhalo alisema malengo yake yalikuwa ni kuibakisha Ligi Kuu KMC na sasa yametimia na anafurahi kwenye hilo.

“Sasa ni kuangalia mbele tujue nini kinafuata hili limeisha na namshukuru mungu umekuwa msimu mzuri kwangu,” alisema Shikhalo ambaye aliizungumzia Ligi Kuu iliyoisha; “Kwa ujumla ilikuwa na ushindani mkubwa timu zilisajili na lazima tukubali wadhamini Azam wameongeza kitu ndio maana kumekuwa na ushindani.”

Soma Pia | Aziz KI Kutua Yanga Muda Wowote

Kipa huyo alisifia uwezo wa nyota wa Dodoma Jiji aliouonesha katika mechi yao ya kufungia msimu ambao KMC ililala bao 1-0 na kumtaja straika Anuary Jabir, aliyesema ni mshambuliaji mzuri na ni msumbufu kwa mabeki.

“Ni Straika mzuri, pia Sadala (Lipangile) na Chikupe (Andrew) wamejitahidi sana kumkaba ndio hivyo mwisho wa siku lazima ukubali ni straika mzuri alitupa wakati mgumu ni kijana mwenye kuweza kufika mbali zaidi,” alisema.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments