Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba SC Yamalizana na Che Fondoh Malone

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Uongozi wa Simba SC leo umemalizana na Beki Che Fondoh Malone mwenye umri wa miaka 24 anayecheza Coton Sport FC kutoka nchini Cameroon kufuatia mazungumzo kati ya Simba SC na Coton Sport FC kwenda vizuri.

Taarifa za kina tulizo nazo ni kuwa, Simba SC iliwasilisha ofa ya pili kwa ajili ya Beki huyo, baada ya ile ya awali kukataliwa, na sasa mazungumzo ya usajili wa Malone yanakwenda vizuri.


Ofa ya pili ya Simba SC inadaiwa kufikia Dola za Marekani 150,000, ambazo ni sawa na Sh. milioni 359.5 za Tanzania, ili kuvunja mkataba wa Malone.

Tayari Uongozi wa Simba SC ulishakubaliana na mchezaji kuhusu mshahara na mambo mengine binafsi ya kimkataba.

Post a Comment

0 Comments