Ticker

6/recent/ticker-posts

Cesc Fabregas ajutia kuhama Arsenal na kujiunga Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Aliyekuwa nyota wa Arsenal, Cesc Fabregas amekiri kuwa anajutia kutengana na Gunners na kujiunga na mabingwa wa Uhispania, Barcelona. 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, alichezea Gunners kwa miaka minane akishiriki zaidi ya michezo 300 na hatimaye kutawazwa nahodha wa timu hiyo. 

Tangu ajiunge na mabingwa hao mara 13 wa Ligi Kuu ya Uingereza, mwaka wa 2003, kiungo huyo wa kati alikuwa katika kikosi cha Arsene Wenger kilichoweka historia. 

Lakini Fabregas aliamua kuhama Gunners na kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Barcelona. 

Baada ya kukaa kwa miaka mitatu Camp Nou, Fabregas alirejea tena Uingereza kutia saini na Chelsea wakati huo chini ya Jose Mourinho mwaka wa 2014 baada ya klabu yake ya zamani ya Arsenal kukataa ofa ya kumnunua. 

Ajutia Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania alifunga mabao 35 katika mechi 129 akiwa na La Blaugrana, lakini halinyimwa nafasi ya kipaumbele katika safu ya kati huku wachezaji Xavi Hernandez, Andres Iniesta na Sergio Busquets wakipendelewa zaidi. 

Akizungumza kwenye mahojiano na Kammy and Ben’s Proper Football Podcast, Mhispania huyo amefichua kwamba sasa anajutia kuhamia katika kambi ya Camp Nou. "Nikiangalia nyuma, labda ningesubiri kidogo, hadi Xavi afunge kidogo, kisha niende huko kuchukua nafasi yake. 

Hata hivyo, kuchanganyikiwa kwa miaka mingi bila kushinda Arsenal kulizidi kunishinda, na nikaamua kuondoka," Fabregas alisema. Aliongeza kuwa mafanikio ya kila mara ya Barcelona wakati huo ikifunzwa na Pep Guardiola yalimshawishi kurejea Uhispania. 

"Niliamua kurejea baada ya kuona kila mtu akishinda Barcelona, ​​na kucheza vizuri sana. Pep (Guardiola) pia aliendelea kunipigia simu na kunitumia ujumbe.Niliamua hiyo ndiyo ilikuwa hatua inayofuata kwangu.” 

Cesc Fabregas alishindwa kuficha furaha yake baada ya Arsenal kuitandika Bournemouth kwenye Uwanja wa Emirates.

Post a Comment

0 Comments