Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi haturudii tena makosa dhidi ya US Monastir

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa hawatarudia makosa kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya US Monastir kwa wachezaji wa timu hiyo kusaka matokeo mapema jambo linaoongeza nguvu ya kujiamini na kucheza kwa utulivu.

Timu hiyo inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa hatua ya makundi inasaka pointi tatu ili kufikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali, ina pointi saba kwenye kundi D baada ya kucheza mechi nne.

Mchezo dhidi ya US Monastri  unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 19 huku yanga wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

YANGA yausogelea ubingwa ligi kuu bara

Wakati anahojiwa Nabi alisema kuna ugumu kwenye mashindano ya kimataifa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi hivyo watajitahidi kupata matokeo mapema kuongeza nguvu ya kujiamini.

“Ikiwa tunakutana na timu imara ambayo inahitaji matokeo ni lazima tufanye kazi kubwa kwenye kutumia nafasi hasa zile za mwanzo zitatufanya tuwe imara na kupata matokeo mazuri.

“US Monastir ni timu imara ina wachezaji wazuri hata wachezaji wetu nao ni wazuri hivyo makosa ambayo tulifanya kwenye mchezo uliopita tunayafanyia kazi,” alisema Nabi.

Post a Comment

0 Comments