Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi Afunguka wachezaji walicho mwambia kabla ya mechi dhidi ya TP Mazembe

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefunguka na kuweka wazi ambavyo wachezaji wake walivyokuwa wanataka kucheza mechi dhidi ya TP Mazembe huku wakimwambia kwamba watashinda mechi hiyo.


Nabi alisema yeye na wasaidizi wake walikuwa katika wakati mgumu kuamua nani ataanza katika mchezo huo kufuatia morali ya juu ambayo wachezaji wake walikuwa nayo ikiwa ni tofauti tangu aanze kuifundisha Yanga.


"Kipindi chote cha maandalizi kilikuwa ni kipindi cha maajabu, kila mchezaji alikuwa anataka kucheza hii mechi, wako wachezaji walikuwa wananipigia mpaka simu wakiniomba kocha nifikirie nicheze hii mechi Yanga tunashinda,"alisema Nabi.


"Kuna mchezaji alinifuata na kuniomba nimpange nafasi tofauti na ambayo tunampanga, na wote wanakwambia tunakwenda kushinda lakini hata mazoezini kulikuwa na morali ambayo sidhani kama nimewahi kuiona tangu nifike hapa Yanga.


"Hii ni maana kwamba wachezaji walijua walikosea wapi kule Tunisia na walitaka kurudisha tabasamu kwa mashabiki wao na viongozi, hata tuliposhinda walinifuata na kuniambia kocha watu wetu wameefurahi.


Aidha Nabi aliongeza kuwa ushindi huo unakwenda kurudisha heshima sio tu Tanzania Bali Afrika wakithibitisha kwamba hawakuifunga Club Africain kwao kwa kubahatisha.


"Tuna timu bora changamoto zilizopo jukumu kubwa ni kuzikabili na kutafuta akili mpya,wapo ambao walidhani Yanga ilibahatisha kushinda mbele ya Club Africain, hii inathibitisha kwamba tuna kikosi imara sio tu hapa ndani bali hata Afrika tunahitaji heshima kwa kiwango chetu.


Katika Mchezo huo Yanga iliichapa Mazembe kwa mabao 3-1 ukiwa ni ushindi wa kwanza wa Yanga dhidi ya klabu hiyo, huku matokeo hayo yakiipa pointi tatu za kwanza katika mechi za Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa wanashika nafasi ya pili katika kundi D.



KUHUSU KMC NA REAL BAMAKO 

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji ameongeza kuwa ushindi ambao wameupata mbele ya Mazembe ni gia ya kuanza safari yenye kasi kupata ushindi zaidi.


Arafat alisema baada ya Mazembe sasa wanawataka wachezaji wao kuigeukia mechi ya Ligi dhidi ya KMC na kushinda vizuri kabla ya kuanza hesabu zingine za kuwafuata Real Bamako ya Mali, katika mechi yao ya tatu ya hatua ya makundi.


"Tulikuwa na Imani kubwa na kauli za wachezaji wetu, kila tulipozungumza nao walisema wanaisubiri Mazembe kazi wamemaliza,"alisema Arafat


"Sasa kazi inayofuata ni kukimbia zaidi, hii ni gia ya kuondokea safari inaanzia hapa anayefuata Sasa ni KMC tumewaambia wachezaji tunatakiwa kuendeleza moto wa ushindi wetu.


"Uongozi tuko mbali tunacheza ligi na wengine wameshaanza hesabu za kuwafuata Real Bamako tunataka kwenda kushinda kule,tunajua na wachezaji wanajua walikosea wapi tulipokwenda Tunisia. 


Mudathir Yahaya afunguka kuisaidia Yanga katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe


Post a Comment

0 Comments