Ticker

6/recent/ticker-posts

Mudathir Yahaya afunguka kuisaidia Yanga katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kiungo Mudathir Yahaya, amesema amejisikia faraja kuifungia timu yake ya Yanga katika ushindi wa mabao 3-1 walio Upata dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza mchezo uliopita.


Yanga ilitoka kifua mbele dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ikiwa ni wiki moja tangu ipoteze mchezo wake wa kwanza wa hatua hiyo ya makundi, ikiwa ugenini dhidi ya US Monastir ya Tunisia.


Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda dakika ya saba, Mudathir Yahya dakika ya 11 na winga Mkongomani Tuisila Kisinda dakika za nyongeza huku bao pekee la Mazembe likifungwa na Alex Ngonga dakika ya 80.


Kwa matokeo hayo, Yanga sasa inashika nafasi ya pili kwenye  msimamo wa Kundi D la Kombe la Shirikisho barani Afrika ambalo kinara ni US Monastir ikiwa na alama nne, TP Mazembe nafasi ya tatu kwa pointi zao tatu, huku Real Bamako ikiburuza mkia baada ya kuambulia alama moja tu katika michezo miwili ambayo kila timu imecheza.


Wakati Akihojiwa Mudhathir alimshukuru Mungu kwa timu yake kuweza kupata alama tatu dhidi ya TP Mazembe, ambazo  zimewasaidia kuwa katika nafasi nzuri.


"Ndio nimerudi uwanjani, nimejisikia faraja kubwa kupata pointi tatu hizi nyumbani kwa sababu tumeshapoteza mchezo uliopita, pointi hizi zitatusaidia, tumekuja tumejipanga, tunamshukuru Mungu alhamdulilah kwa hilo," alisema Mudathir.


Mchezo mwingine wa Kundi D, ulizikutanisha timu za Real Bamako na US Monastir ambapo matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.


Yanga itashuka tena dimbani Jumapili wiki hii ambapo itakuwa ugenini nchini Mali dhidi ya vibonde wa kundi hilo, Real Bamako, wakati TP Mazembe ikiwakaribisha US Monastir jijini, Lubumbashi.

   

Post a Comment

0 Comments