Ticker

6/recent/ticker-posts

Mastaa Yanga wapewa Sh130 milioni baada ya kuifunga TP Mazembe

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Baada ya Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe mastaa wa kikosi cha Yanga wamepewa kitita cha Sh130 milioni kwa soka safi na la kuvutia walilopiga juzi.


Mapema baada ya mchezo huo kumalizika timu hiyo kabla haijaondoka uwanjani wachezaji wa Yanga walijichukulia sh 33 milioni keshi zikitolewa na wadau mbalimbali.


Msemaji wa Serikali Greyson Msigwa alisema uwanjani hapo juzi kuwa kiasi Cha Sh 15 kimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitekeleza kwa vitendo ahadi yake ya kulilipia kila bao moja sh 5 milioni.


Yanga kwa mabao hayo matatu walikabidhiwa hapo hapo kiasi Cha sh 15 milioni, zilizoletwa na Msigwa mwenyewe huku akiwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pindi Chana kisha kupokelewa na Rais wa Yanga injinia, Hersi Said.


"Fedha zingine zimetolewa na ahadi ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye alisema kila bao atalilipia shilingi milioni moja na kufanya jumla ametoa milioni tatu, zingine ametoa waziri wa fedha Mwigulu Nchemba na zingine Chama Cha soka DRFA,"alisema Msigwa.


"Kuna zingine zimetoka Wizara ya Maliasili na Utalii na zingine Wizara ya michezo kwa hiyo jumla tumewapa milioni thelathini na tatu."


Wakati wadau wakikabidhi fedha hizo bonasi kubwa itatoka kwa uongozi wa Yanga na mfadhili wao GSM ambaye aliwaahidi kiasi cha 100 milioni kama watashinda mchezo huo.


"Tumepata fedha ndugu yangu, mara nyingi kwenye soka ukishinda unakutana na hali kama hii, tumevuna nafikiri zaidi ya milioni 130 jinzi ambavyo tumeelezwa hii ni motisha kubwa sana kwetu," alisema mchezaji mmoja aliyeomba asitajwe jina.


Hii itawafanya wachezaji hao kujihakikishia kuweka mfukoni jumla ya Sh 133 milioni kufuatia ushindi wao huo wa kwanza wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mazembe ikiwa ni zile zinazofahamika ukiacha zile ambao wadau wamekuwa wakituma wenyewe.


Huu ni ishindi wa Yanga wa kwanza wa hatua ya makundi baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Monastir kulala kwa mabao 2-0 ugenini, sasa Yanga wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao ambalo linaongozwa na Monastir wenyewe pointi nne, wakifuata wakiwa na tatu sawa na Mazembe na Real Bamako wana pointi tatu.


Yanga sasa watasafiri kuwafuata Bamako Mali baada ya hapo watarudi nyumbani kucheza na timu hiyohiyo kwenye Dimba la Mkapa na kama wanataka kuhakikisha wanakuwa na nafasi nzuri ya kufuzu wanatakiwa kushinda michezo hiyo yote miwili.


Nabi Afunguka wachezaji walicho mwambia kabla ya mechi dhidi ya TP MazembePost a Comment

0 Comments