Ticker

6/recent/ticker-posts

MORRISON NJE MIEZI MIWILI YANGA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Daktari wa timu ya Yanga, Moses Etutu amethibitisha kuwa wachezaji wawili Abutwalib Mshery pamoja na Bernard Morrison watakuwa nje ya kikosi hicho kwa muda wakiuguza majeraha tofauti.


Akizungumza na YANGA MEDIA, Daktari Moses alisema kuwa kipa wao, Abutwalib Mshery atakuwa nje kwa takribani miezi 3-4.


“Mshery ana tatizo la goti kitaalamu inaitwa “meniscus grade 2 tear” ambapo ataenda kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia na baada ya hapo atarejea kwa ajili ya uangalizi wa karibu,” amesema Dk. Etutu.


Kwa upande mwingine, Dk. Etutu pia amezungumzia kuhusu mchezaji Bernard Morrison ambae nae yupo nje kwa muda mrefu.


“Morrison ana tatizo la nyama za paja (pubalgia) na atakuwa nje kwa muda wa miezi miwili, na ameshaanza kutibiwa mpaka sasa akiwa ameshakamilisha asilimia 40% ya matibabu yake,” amesema Dkt. Etutu.


Aidha, Morrison anatibiwa na ataendelea kutibiwa hapa hapa nchini Tanzania kwani tatizo lake ni kawaida na linawezekana kutibiwa nchini bila kwenda nje ya nchi.


Post a Comment

0 Comments