Ticker

6/recent/ticker-posts

Jezi Mpya Ya Simba Ligi Ya Mabingwa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

KLABU ya Simba jana usiku imezindua jezi maalum kwa ajili ya Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zimebeba ujumbe wa kuitangaza Tanzania.


Simba itacheza mechi yake ya kwanza ya Kundi C Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji, Horoya Jumamosi Uwanja wa Jénérali Lansana Conté Jijini Conakry, Guinea.


Baada ya hapo, Simba itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili dhidi ya Raja Casablanca Februari 18, kabla ya kwenda kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kuchuana na Vipers ya Uganda Februari 25 Uwanja wa St. Mary’s, Kitende mjini Entebbe.


Mechi za mzunguko wa pili Simba itaanzia nyumbani dhidi ya Vipers Machi 7, kabla ya kuwakaribisha Horoya Machi 17 na kuwafuata Raja Casablanca Machi 31.Post a Comment

0 Comments