Ticker

6/recent/ticker-posts

VIDEO: Jezi Mpya Za Simba Msimu Wa 2022/23

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Jezi Mpya Za Simba Msimu Wa 2022/23 zinapatikana kwa Tsh. 35,000 tu kwenye duka la Vunja Bei Sinza Madukani.

Leo August 7,2022 Simba imezindua JEZI mpya ambazo zinatarajiwa kutumika kwa msimu wa 2022/23.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kuwa uzi huo kwa sasa unapatikana Dar es Salaam kwanza wakati mchakato ukiwa unaendelea ili ziweze kupatikana nchi nzima.

“Jezi yetu mpya ambayo tumeizindua kwa sasa inapatikana Dar es Salaam kwa wakazi wa mikoani wasiwe na shaka uzi wetu utafika kila sehemu ambapo wapo maduka ya vunja bei yapo.

“Bei rasmi ya Jezi inapatikana kwa Tsh. 35,000 tu kwenye duka la Vunja Bei Sinza Madukani.” .

TAARIFA RASMI KUTOKA KLABU YA SIMBA
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye leo tumezindua jezi mpya ambazo tutazitumia katika mashindano yote ndani ya Msimu wa Ligi 2022/23.

Jezi zetu zipo kwenye ubora mkubwa kuanzia zilivyotengenezwa kimwonekano

Jezi zilizozinduliwa ziko aina tatu kama kawaida yaani ya nyumbani (nyekundu), ugenini (nyeupe) na jezi namba tatu (kijivu).

Baada ya uzinduzi huu wa jezi zitaanza kuuzwa katika maduka yote ya Vunjabei nchi nzima ambapo Wanasimba wataenda kununua kwa ajili ya mtoko husani wa kesho kwenye Tamasha letu la Simba Day.

Tunawaomba Wanasimba kununua jezi kwa wingi ili kesho kwenye Tamasha letu pale Benjamin Mkapa tupendeze kama kawaida yetu.
 
VIDEO: Jezi Mpya Za Simba Msimu Wa 2022/23


 
Post a Comment

0 Comments