Ticker

6/recent/ticker-posts

Sakho, Baleke kuwavaa Horoya Ligi ya Mabingwa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

   

Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi  Ligi ya Mabingwa Afrika klabu ya Simba imewatoa hofu mashabiki na wanachama wa timu hiyo, kuhusu kuwakosa nyota wawili wa kikosi cha kwanza Pape Sakho na Jean Baleke baada ya kushindwa kumaliza mechi dhidi ya Al Hilal ya Sudan.


Katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Sakho alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata maumivu ya mguu wakati Baleke alitolewa uwanjani kwa machela hali iliyozua hofu kwa mashabiki wa Simba kuelekea mechi dhidi ya Horoya AC nchini Guinea Jumamosi wiki hii.


Daktari wa Simba, Edwin Kagabo, amesema nyota hao hawakupata madhara makubwa na wanaendelea vizuri, hivyo watajiunga na wenzao mazoezini.


"Sakho na Baleke walipata maumivu katika mchezo wa Al Hilal, lakini hawakupata madhara makubwa, wanaendelea vizuri na wataendelea na programu ya mazoezi," alisema Dk. Edwin


Katika hatua nyingine kiungo Sadio Kanoute naye atarejea uwanjani baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars, uliopigwa Ijumaa iliyopita.


Kanoute alitolewa dakika ya 83 ya mchezo baada ya kupata maumivu hayo hali iliyozua hofu kwa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo, lakini nyota huyo raia wa Mali hakupata madhara makubwa.


Kwa mujibu wa Daktari wa Simba, Kagabo, Kanoute aliangukia nyonga na kupata maumivu yaliyofanya ashindwe kuendelea na mchezo, lakini halikuwa tatizo kubwa.


Moses Phiri Aahidi Makubwa Baada Ya Kurejea UwanjaniPost a Comment

0 Comments