Ticker

6/recent/ticker-posts

Kylian Mbappe Yuko Tayari Kukatwa Mshahara Kuondoka PSG

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Kylian Mbappé amesema yuko tayari kukatwa mshahara wake katika klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ili kuachana na mabingwa hao wa Ufaransa mtandao wa Sportskeeda umeripoti.


Mbappe anaripotiwa kuwa tayari kuachana na mabingwa hao wa Ligue 1 msimu ujao wa joto na atawasilisha uamuzi wake kwa bodi ya PSG. 


Mbappe amekuwa kiungo muhimu wa PSG tangu alipojiunga nao mwaka wa 2017 huku akiwafungia mabao 191 katika mechi 238 katika michuano yote.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, anasemekana kutofurahishwa na uongozi wa PSG kwa kutotimiza ahadi zake baada ya kumshawishi kukataa ofa ya Real Madrid na kusalia Paris. 


Kulingana na Sportskeeda, Mbappe sasa ameamua kulazimisha kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu na yuko tayari kukubali kukatwa mshahara.


Mshindi huyo wa kiatu cha dhahabu cha Kombe la Dunia 2022, pia anatazamia kunawiri katika taalamu yake kwingineko kwani Mfaransa huyo anaamini kwamba amefanikisha kila alichokihitaji katika klabu hiyo ya Ligue 1. 


Real Madrid wanaripotiwa kwamba bado wana hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Monaco licha ya kukataliwa na Mbappe hapo awali na pia wako tayari kulipa PSG kitita kikubwa cha pesa.


Wakati huo huo, nyota wa zamani wa Real Madrid, Jese Rodríguez Ruiz amefichua kuwa Kylian Mbappe alishinikizwa kurefusha mkataba na PSG msimu huu wa joto, Gist Reel inaripoti. 


Mbappe alihusishwa na Real Madrid mwaka jana, lakini dili hilo liliambulia patupu baada ya kuamua kutia saini upya na PSG, jambo ambalo pamoja na mambo mengine lilimpa mshahara mkubwa zaidi. 


Awali, Mbappe aliripotiwa kuweka masharti matatu muhimu ili aendele kusalia Paris Saint-Germain, moja ya masharti hayo ikiwa ni pamoja na PSG kumuuza nyota wa Brazil, Neymar. 


Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumapili 01.01.2023


Post a Comment

0 Comments