Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi Za Soka Barani Ulaya Jumapili 01.01.2023

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

Baba yake Jude Bellingham anataka kiungo huyo wa kati wa Uingereza na Borussia Dortmund ajiunge na Liverpool, huku Real Madrid na Manchester City pia wakisaka saini ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)


Aston Villa wanafuatilia hali ya mlinda mlango wa Everton na England Jordan Pickford, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado hajasaini mkataba mpya huku akiwa amebakiza zaidi ya mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa Goodison Park. (Sun)


Chelsea wamepiga "hatua moja" kumsajili kiungo wa kati wa Benfica na Argentina Enzo Fernandez, 21. (Relevo - kwa Kihispania)


Mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 23 - anayelengwa na Manchester United - yuko tayari kuondoka Atletico Madrid mwezi Januari. (GiveMeSport)


Klabu ya MLS ya Sporting Kansas City ilijaribu kumsajili Cristiano Ronaldo kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia. (Fabrizio Romano)


Newcastle wametoa "ofa kubwa sana" kwa mlinzi wa Real Madrid Ferland Mendy, 27. (Foot Mercato)


Chelsea wanajaribu kumsajili beki wa Ufaransa Benoit Badiashile lakini mkufunzi wa Monaco Philippe Clement ameonya kuwa sio klabu pekee inayojaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Metro)


Mykhailo Mudryk anasema mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ni "kocha bora", huku Chelsea ikiungana na The Gunners katika kinyang'anyiro cha kumnasa winga huyo wa Shakhtar Donetsk mwenye umri wa miaka 21. (Metro)


Tottenham Hotspur "imechukua hatua za kwanza" katika mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Sporting Lisbon ya Uingereza Marcus Edwards, 24. (A Bola, kupitia TeamTalk).


Spurs pia wanakaribia kukamilisha dili la £35m kwa mlinzi wa Sporting Lisbon Pedro Porro, 23. (Star).


Tottenham wako tayari kumuuza beki wa kulia wa Brazil Emerson Royal mwenye umri wa miaka 23 baada ya kuto tokea uwanja wa mazoezi. (Football Insider)


Kipa wa Morocco Yassine Bounou, 31, anaweza kuondoka Sevilla na kwenda Manchester United au Bayern Munich mwezi Januari. (Foot Mercato - kwa Kifaransa)


Leeds United wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili beki Maximilian Wober, 24, kutoka Red Bull Salzburg. (90 min)


Mshambulizi wa Borussia Monchengladbach na Ufaransa Marcus Thuram, 25, angependelea kujiunga na Manchester United kuliko Newcastle au Aston Villa, ambao pia wanavutiwa. (Bild - kwa Kijerumani)


Los Angeles FC wameshinda vilabu vinavyovutiwa na Premier League kumsajili fowadi wa Croatia Stipe Biuk, 20. (Daily Mail)


Juventus wanavutiwa na kiungo wa kati wa Everton na Mali Abdoulaye Doucoure, 29. (Mtandao wa Calcio Mercato - kwa Kiitaliano)


Kiungo wa kati wa Manchester United wa Tunisia, Hannibal Mejbri, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Birmingham City, anavutiwa na Marseille. (Sun)


Tetesi za Soka Barani Ulaya Ijumaa 23.12.2022


Post a Comment

0 Comments