Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea Yakubali Kutoa €38m Kukamilisha Usajili Wa Benoit Badiashile Wa Ufaransa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 

KLABU ya Chelsea wamefikia makubaliano na Klabu Monaco ya nchini Ufaransa ili kusaini Benoit Badiashile mwenye miaka 21 kwa dau la euro milioni 38, kwa mujibu wa mtandao wa The Athletic.


Tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Chelsea wamekuwa bize sokoni kusaka wachezaji ambapo mbaka sasa tayari wamefanikiwa kuzinasa saini za wachezaji David Datro Fofana na Andrey Santos, huku wakiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Badiashile.


Mlinzi huyo wa upande wa kushoto amekuwa kwenye rada za Chelsea kwa muda mrefu sasa. Hapo awali waliusishwa na Josko Gvardiol, lakini siku za hivi karibuni wameamua kuelekeza mawazo yao kwa Badiashile.


Chelsea kwa muda mrefu wamekuwa katika mazungumzo na Monaco juu ya mpango wa kumsajili Badiashile na sasa juhudi zao, zinaonekana kufanikiwa.


Kwa mujibu wa mtandao wa The Athletic, Chelsea wamefikia makubaliano kamili na Monaco kumsaini Badiashile. Sasa wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa Ada yenye thamani ya karibu € 37-38 milioni.


Chelsea tayari imejiandaa kumpokea Badiashile mwenye umri wa miaka 21 tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na wenzake Stamford Bridge, kama inavyo ripotiwa. 


Mchezaji huyo sasa anatarajiwa kusaini kandarasi ya muda mrefu na Blues hadi 2029.


Badiashile ametokoa katika timu ya vijana ya Monaco kwa mara ya kwanza aliichezea Monaco katika mechi ya ligi kuu dhidi ya PSG na kushuhudia Monaco ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na PSG mnamo Novemba 2018. Tangu wakati huo ameichezea monaco michezo 135 katika mashindano yote ya Ligue 1, akihusika katika mabao tisa.


Badiashile ni miongoni mwa vijana ambao Chelsea wamekuwa wakiwatazama kwa muda mrefu huku wakiwemo Evan N'dicka wa Eintracht Frankfurt's na Piero Hincapie wa Bayer Leverkusen's zote za ujerumani.


Mfaransa huyo sasa ataongeza machaguo zaidi kwa kocha Potter katika safu ya ulinzi ya Chelsea, ambayo tayari ina Thiago Silva, Kalidou Koulibaly, Wesley Fofana, na Trevoh Chalobah.


Kylian Mbappe Yuko Tayari Kukatwa Mshahara Kuondoka PSG

Post a Comment

0 Comments