Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Morocco Watoshana Nguvu Na Croatia Katika Mechi Ya Kundi F

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

WANAFAINALI wa Kombe la Dunia 2018, Croatia, walianza kampeni zao za mwaka huu nchini Qatar kwa sare tasa dhidi ya Morocco ugani Al Bayt.

Ni wachezaji wanne pekee waliounga kikosi cha Croatia kwenye fainali za 2018 ambao waliwajibishwa dhidi ya Morocco waliokosa kunogesha makala manne ya awali ya Kombe la Dunia hadi 2018 nchini Urusi.

Huku Croatia ambao ni w 12 kimataifa wakitegemea zaidi maarifa ya Luka Modric na Mateo Kovacic, Morocco walichuma nafuu kutokana na kasi ya nahodha Romain Saiss aliyeshirikiana vilivyo na Achraf Hakimi, Nayef Aguerd, Youssef En-Nesyri na Hakim Ziyech.

Watano hao walimwajibisha vilivyo kipa wa Croatia, Dominik Livakovic. Sare iliyosajiliwa na Morocco dhidi ya Croatia ilkuwa ya kwenye fainali za Kombe la Dunia kufikia sasa mwaka huu – Denmark walianza kampeni za Kundi D kwa sare tasa dhidi ya Tunisia huku Poland na Mexico wakitoshana nguvu kwa sare tasa nyingine katika Kundi C.

Ni mechi moja pekee iliyokamilika kwa sare tasa kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2018 nchini Urusi. Croatia wameratibiwa kuvaana na Canada mnamo Novemba 27 huku Morocco wakichuana na Belgiji siku hiyo hiyo.

Morocco walishuka dimbani dhidi ya Croatia wakijivunia rekodi nzuri ya kutopigwa katika mechi tano mfululizo. Walikomoa Chile (2-0) na Georgia (3-0) kabla ya kuambulia sare tasa dhidi ya Paraguay mnamo Septemba 2022.

Kikosi hicho kinachokamata nafasi ya 22 duniani, sasa kinanolewa na kocha Walid Regragui ambaye ana kibarua kizito cha kuongoza masogora wake kukahimili ushindani mkali wa Kundi F linalojumuisha pia Ubelgiji na Croatia waliopigwa na Ufaransa 4-2 kwenye fainali ya 2018 jijini Moscow, Urusi.

Post a Comment

0 Comments