Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Macho Yote kwa Neymar na Ronaldo, Brazil na Ureno Zikianza Dimba la Kombe la Dunia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Cristiano Ronaldo anatakiwa kusahau masaibu yake ya kutimuliwa Manchester United akiongoza Ureno kwenye mechi dhidi ya Ghana 
  • Neymar naye anategemewa na Brazil kukabiliana na kikosi hatari cha Serbia wakati timu hizo zitakapokutana leo 
  • Brazil watakuwa wanasaka kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya sita 


Brazil wataanza leo Alhamisi, Novemba 24, kampeni zao za kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya sita watakapovaana na Serbia. 

Wakati huo huo Cristiano Ronaldo anatarajiwa kusahau masaibu yake ya kutimuliwa Manchester United akiongoza Ureno kwenye mechi dhidi ya Ghana. 

Brazil watakuwa makini kukabiliana na kikosi hatari cha Serbia wakati timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa Lusail. 

Wasiwasi inatawaliwa haswa na kushuhudia Argentina ikipokezwa kichapo cha kushtukiza dhidi ya Saudi Arabia mnamo Jumanne, Novemba 22 huku Ujerumani pia wakitandikwa na Japan Jumatano, Novemba 23. 

Kikosi cha Tite kinaweza kumtegemea Neymar ambaye amekuwa katika hali mbaya sana akichezea klabu ya Paris Saint-Germain. 

Hata hivyo, mchezaji mghali zaidi duniani, anawashambuliaji wengine mahiri walio tayari kubeba mzigo huo kama vile Vinicius Junior na Rodrygo wa Real Madrid. 

"Kwa maoni yangu wachezaji hawa watamsaidia Neymar kwa sababu wanaweza kugawanya majukumu na kutengeneza nafasi kwa ajili yake." 

"Hali katika kikosi ni nzuri sana. Mchanganyiko wa wachezaji chipukizi na wenye uzoefu zaidi unaleta muunganisho mkubwa," alisema nahodha mkongwe wa Brazil Thiago Silva 

Hata hivyo, Serbia wanaonekana kuwa hatari zaidi kuliko miaka minne iliyopita, walipokutana pia na Brazil katika hatua ya makundi japo walipigwa 2-0 na kuondolewa katika raundi ya kwanza. 

"Hatuogopi mtu yeyote duniani, hata Brazil," alisisitiza kocha wa Serbia, Dragan Stojkovic. 

Ronaldo 

Kwa upande mwingine, maandalizi ya Ronaldo kwa kile ambacho mchuano wake wa mwisho wa Kombe la Dunia, yamegubikwa na masaibu ya kulazimishwa kuondoka Old Trafford. 

Kiwango chake katika klabu ya Man United msimu huu, kimekuwa hafifu lakini bado ana matumaini ya kupata kujikwamua katika michuano ya Kombe la Dunia. 

Ureno inatarajiwa kuanza kwa ushindi dhidi ya Ghana katika nafasi ya 61 kulingana na viwango vya FIFA. 

Kocha wa Ureno Fernando Santos alidai kuwa kutengana kwa Ronaldo na United hakujajadiliwa na wachezaji. 

Ureno na Ghana ziko Kundi H pamoja na Uruguay na Korea Kusini. 

Post a Comment

0 Comments