Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Japan Wazamisha Chombo Cha Ujerumani Kwa Kichapo Cha 2-1 Katika Mechi Ya Kundi E

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

JAPAN walitoka nyuma na kufunga mabao mawili ya haraka mwishoni mwa kipindi cha pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wafalme mara nne wa Kombe la Dunia, Ujerumani, kwenye pambano la Kundi E katika Uwanja wa Khalifa International.

Ingawa Ujerumani walianza mechi kwa matao ya juu, walipoteza nafasi nyingi za wazi.

Fowadi Takuma Asano alitokea benchi na kufunga bao la pili ya Japan katika dakika ya 83, sekunde dakika tano baada ya Ritsu Doan kusawazisha mambo na kufuta juhudi za Ilkay Gundogan aliyewaweka Ujerumani kifua mbele kupitia penalti kunako dakika ya 33.

Bao la Doan lilifungwa baada ya msururu wa mashabulizi katika malango ta vikosi vyote viwili. Kipa Shuichi Gonda wa Japan alijituma maradufu na kupangua makombora mazito aliyoelekezewa na Serge Gnabry na Jonas Hofmann kabla ya mlinda-lango Manuel Neuer naye kumzidi ujanja mshambuliaji Junya Ito.

Ujerumani waliovuta mkia wa kundi lao kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, wangalifunga mabao zaidi wakijivunia uongozi wa 1-0.

Sasa wana kibarua kizito cha kujinyanyua dhidi ya Uhispania mnamo Novemba 27 kabla ya kufunga kampeni za Kundi E dhidi ya Costa Rica siku tatu baadaye.

Kabla ya kipenga cha kuashiria mwanzo wa mechi kupulizwa, wachezaji wa Ujerumani waliweka mikono yao midomoni huku waziri wa taifa hilo, Nancy Faeser, akivalia utepe wenye maandishi OneLove.

Tukio hilo linajiri baada ya Shirikisho la Soka la Ujerumani (DFB) linachunguza iwapo ni haki kwa Shirikisho la Duniani (FIFA) kutishia kuchukulia wachezaji hatia za kisheria kwa kuvalia tepe zenye maandishi ya OneLove nchini Qatar.

Ujerumani almaarufu Die Mannschaft walidenguliwa mapema kwenye fainali za Kombe la Dunia katika hatua ya makundi miaka minne iliyopita huku Japan wakitinga raundi ya 16-bora ambapo waling’olewa na Ubelgiji.

Wakiwa chini ya kocha Joachim Loew wakati huo, Ujerumani walishindwa kutetea kwa mafanikio ubingwa wa Kombe la Dunia walioutwaa mnamo 2014 nchini Brazil baada ya kupepeta Argentina 1-0.

Badala yake, walifungua kampeni za Kundi F kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa Mexico. Japo walitandika Uswidi 2-1 katika mchuano wa pili, walinyolewa kwa 2-0 na Korea Kusini katika pambano la tatu.

Ujerumani ambao ni mabingwa mara nne wa Kombe la Dunia, waling’olewa na Uingereza kwenye hatua ya 16-bora ya fainali zilizopita za Euro 2020 kwa kichapo cha 2-0 ugani Wembley.

Matokeo hayo yalitamatisha kipindi cha ukufunzi wa Loew aliyejiuzulu na nafasi yake kutwaliwa na Hansi Flick aliyeagana na klabu ya Bayern Munich.

Mechi dhidi ya Mexico mnamo 2018 nchini Urusi ilikuwa ya kwanza tangu 1986 kwa Ujerumani kupoteza katika pambano lao la ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia.

Hadi mwaka wa 2018, Japan walikuwa wamezoea kuondolewa katika hatua ya makundi kwenye makala matano mfululizo ya fainali za Kombe la Dunia kuanzia 1998.

Hata hivyo, sasa wanajivunia rekodi nzuri ya kushinda mechi 16 kati ya 19 zilizopita huku wakifunga jumla ya mabao 60. Japan wameshinda michuano sita kutokana na 22 iliyopita kwenye fainali za Kombe la Dunia. Walifungua kampeni zao za makundi mnamo 2018 kwa ushindi wa 2-1

Post a Comment

0 Comments