Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia 2022: Morocco Yaitandika Ubelgiji 2-0 na Kumshtua Romelu Lukaku

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Morocco wamejipatia ushindi wao wa tatu kwenye Kombe la Dunia dhidi ya Ubelgiji huku mabao ya Abdelhamid Sabiri na Zakaria Aboukhlal yakiipa taifa hilo la Afrika ushindi wa kihistoria wa 2-0. 

Sabiri alionja wavu baada ya kumshinda maarifa Thibaut Courtois kwenye lango akitia mpira wa bwerere kimyani kabla ya Aboukhlal kuwasiliana na Hakim Ziyech kupata mpira na kuongeza bao la ushindi katika muda wa lala salama. 

Morocco walinyimwa bao la kwanza katika kipindi cha kwanza wakati Ziyech alifunga goli lililokataliwa na VAR kwa msingi wa kuotea. 

Morocco sasa wanachukua nafasi ya Ubelgiji kileleni mwa Kundi F na watafuzu kwa hatua ya muondoano kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1986 iwapo wataepuka kichapo dhidi ya Canada siku ya Alhamisi, Disemba 1. 

Ubelgiji, ambayo ni timu inayoshikilia nafasi ya pili bora na duniani, nayo italazimika kuwapiga Croatia ili kujihakikishia nafasi katika duru ya 16. 


Jinsi mambo yalivyokuwa 

Ubelgiji walitawala dakika za mapema za mechi lakini Morocco ndiyo walifanikiwa kufungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Hakim Ziyech alipopiga shuti kutoka mbali. 

Mashabiki wa Morocco walizua shangwe kubwa wakati mpira wa adhabu wa Ziyech ulipopaa hadi wavuni katika kipindi cha kwanza. 

Hata hivyo, sherehe yao ilikuwa ya muda mfupi baada ya ukaguzi wa VAR kufutilia mbali bao hilo kwa msingi kuwa Romain Saiss alikuwa ameegemea tuna beki huyo wa zamani wa Wolves alikuwa ameotea kwenye mboni ya 'kipa Courtois'. 

Katika awamu ya pili, timu zote zilianza kwa matao ya juu huku Ziyech akivurumisha shuti iliyokuwa rahisi kwa Courtois kupangua naye Hazard akiondoa hatari ya Munir kwenye lango. 

Sofiane Boufal nusura avunje kimya katika dakika ya 57 baada ya kukimbia kwa kasi lakini akaupinda mpira nje ya lango. 

Martinez alifanya mabadiliko mawili katika dakika za lala salama, akimuondoa Hazard na kumchukua Dries Mertens na kumuingiza Youri Tielemans kwa nfasi ya Amadou Onana katika safu ya kati. 

Sabiri kutoka karibu na mstari wa kugusa, sawa na bao lililotolewa na Ziyech, ukimpata Courtois mwenye mguu gorofa. 

Martinez pia alimchezesha Romelu Lukaku, anayetarajiwa kukosa mechi kadhaa za Kombe la Dunia kwani anauguza jeraha, lakini kuwepo kwake hakukuwa na tofauto yoyote. 

Umahiri wa Ziyech ulibuni nafasi ya wazi kwa Aboukhlal kupenyeza kwenye ngome ya winga huyo wa Chelsea na kupachia mpira wavuni. 

Post a Comment

0 Comments