Ticker

6/recent/ticker-posts

Kombe la Dunia 2022: Ufaransa Yawa Timu Ya Kwanza Kufuzu Hatua Ya 16 Bora nchini Qatar

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Timu ya Taifa ya Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufuzu  raundi ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yanayoendelea nchini Qatar kufuatia ushindi dhidi ya Denmark. 

Ufaransa imefuzu kwa hatua hiyo kufuatia ushindi muhimu wa 2-1 dhidi ya Denmark katika uwanja wa 974, mshambuliaji nyota Kylian Mbappe akifunga mabao yote ya Ufaransa mbele ya mashabiki 24,860. 

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya pili kwa timu zote, ilikataa kufunguka katika kipindi cha kwanza, kila mmoja akimshambulia mwenzake bila mafanikio. 

Mbappe alivunja ubikra wa mechi katika dakika ya 61 alipowapa mabingwa watetezi bao la kuongoza katika dakika ya 61 lakini beki wa Barcelona Andreas Christensen akaswazishia Denmark dakika saba baadaye. 

Mbappe hata hivyo alirejea katika dakika ya 86 na kufunga bao la ushindi kwa vijana wa Didier Deschamps na mechi hiyo kuishia 2-1. 


Ufaransa yafuzu ya kwanza kwa raundi ya 16 bora 

Kwa ushindi huo, Ufaransa sasa ina alama sita katika kundi D baada ya kuicharaza Australia 4-1 katika mechi ya ufunguzi mnamo Jumanne - Novemba 22. 

Ufaransa sasa imekuwa timu ya kwanza kuingia raundi ya 16 bora licha ya kuwa na mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Tunisia mnamo Novemba 30. 

Denmark nayo baada ya sare tasa dhidi ya Tunsia kwenye mechi ya ufunguzi, inahitaji kuitandika Australia katika mechi yao ya mwisho ya makundi mnamo Novemba 30 ili kufuzu kwa raundi ya 16 bora. 

Post a Comment

0 Comments