Ticker

6/recent/ticker-posts

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Costa Rica Yaitandika Japan 1-0 Katika Mechi Ya Kundi E

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

JAPAN walishindwa kuendeleza ubabe uliowavunia ushindi wa 2-1 dhidi ya Ujerumani katika mechi ya kwanza ya Kundi E kwa kuruhusu Costa Rica kuwafunga 1-0 katika pambano la pili katika dimba la Ahmad Bin Ali.

Bao la pekee katika mchezo huo kati ya Japan na Costa Rica lilijazwa wavuni na Keysher Fuller katika dakika ya 81.

Matokeo hayo yanaacha Japan na Costa Rica wakiwa na alama tatu kila mmoja katika Kundi E linalojumuisha pia Uhispania na mabingwa mara nne, Ujerumani.

Baada ya kutandika Ujerumani katika pambano la ufunguzi wa Kundi E, Japan walishuka dimbani dhidi ya Costa Rica wakipigiwa upatu wa kushinda ikizingatiwa kwamba wapinzani wao walinyeshewa mvua ya mabao 7-0 na Uhispania – mabingwa wa Kombe la Dunia 2010 watakaofuzu kwa hatua ya 16-bora iwapo watakomoa Ujerumani katika mchuano wa pili mnamo Novemba 27.

Hata hivyo, mbinu ya kocha wa Japan, Hajime Moriyasu, kukifanyia kikosi kilichovaana na Ujerumani mabadiliko matano ilikosa kuzaa matunda.

Post a Comment

0 Comments