Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yamtoa Ngushi CAF

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji Crispin Ngushi hatoichezea Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya klabu hiyo kutosajili jina lake litumike katika mashindano hayo msimu huu.

Mshambuliaji Crispin Ngushi hatoichezea Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya klabu hiyo kutosajili jina lake litumike katika mashindano hayo msimu huu.

Orodha iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikionyesha usajili wa Yanga kwa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, haina jina la Ngushi huku ikifafanua kuwa klabu yake haijamjumuisha.

Kikosi hicho cha wachezaji 27 waliosajiliwa kinaundwa na makipa Abutwalib Mshery, Johora Erick na Djigui Diarra wakati mabeki ni Hamad Ibrahim,David Brayson,  Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Lomalisa Mutambara, Kibwana Shomari, Djuma Shaban na Abdallah Shaibu.

Viungo ni Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Salum Abubakar, Faridi Musa, Feisal Salum, Yannick Bangala, Aziz Ki na Ducapel Moloko wakati washambuliaji ni Yusuph Athuman, Fiston Mayele, Bernard Morrison, Lazarous Kambole, Denis Nkane, Heritier Makambo na Dickson Ambundo

Post a Comment

0 Comments