Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA KMC FC YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 KWA MKAPA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na KMC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Bao la dakika ya 89 lililofungwa na mchezaji wa akiba Habib Kyombo liliinusuru klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi kwa pointi moja, hivyo kuwa sare yao ya kwanza kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu .

Wekundu hao walikuwa wa kwanza kuandika bao la mapema kupitia mshambuliaji wao Mzambia Moses Phiri ambaye hadi sasa ameifungia timu yake mabao matatu katika mechi tatu Alizocheza.

Licha ya bao lake kudumu katika kipindi chote cha kwanza, KMC ilisawazisha bao hilo dakika ya 48 kupitia Matheo Antony kabla ya George Makang’as kuongeza bao la pili dakika ya 57.

Hata hivyo, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa KMC kuchukua pointi moja kutoka kwa Simba kwani katika mechi nane walizokutana kati yao, timu hiyo imekuwa ikipoteza mara nyingi mbele ya Simba.

Pia, KMC wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutikisa nyavu za Simba kwani kabla ya mchezo huo, wababe hao wa mtaa wa Msimbazi nyavu zao zilikuwa hazijatikiswa katika mechi zao mbili awali za Ligi Kuu.

Jumamosi ya septemba 10, Simba itamenyana na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Bingu mjini Lilongwe .

Post a Comment

0 Comments