Ticker

6/recent/ticker-posts

Mashabiki wamkataa Matola kwa Mkapa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

WAKATI mpira ukiendelea uwanja wa Mkapa na Simba kuwa nyuma kwa mabao 2-1, mashabiki wametoa ya moyoni juu ya kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola'Veron'

Ilikuwa ni dakika ya 75 wakati mchezo umesimama huku baadhi ya wachezaji wakipatiwa huduma ya kwanza, mashabiki wa jukwaa la kaskazini walisikika wakiimba kuwa hawamtaki Matola.

Mashabiki hao waliosikika wakiimba;  "Hatumtaki, Matolaa, hatumtaki Matola" mbali ya wimbo huo pia walionyesha ishara ya kukataa kwa mikono.

Matola analiongoza benchi la Simba baada ya timu hiyo kuachana na kocha wao mkuu Zoran Maki mapema jana, Jumanne, baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Post a Comment

0 Comments