Ticker

6/recent/ticker-posts

Graham Potter alia na safu ya ushambuliaji, Chelsea

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha wa Chelsea Graham Potter amesema hajapendezwa na matoko ya sare ya bao 1-1 waliyoyapa dhidi ya RB Salzburg kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya jana usiku. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza Potter anakiongoza kikosi che The Blues akiwa kocha mkuu.

Graham Potter ameshuhudia kibarua chake cha kwanza akiwa kocha wa Chelsea na mchezo wake wa kwanza na wa pekee kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya ukimalizika kwa sare. Katika mchezo huo Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Raheem Sterling dakika ya 48 na baadae dakika ya 75 Salzburg wakasawazisha kupitia kwa Noah Okafor.

Baada ya mchezo huo Potter ameweka wazi kuwa hajapendezwa na matokeo hayo huku akisisitiza kuwa hawakuwa bora eneo la ushambuliaji.

‘’Nimesikitishwa na matokeo ya mwishoni. Nadhani wachezaji wangu walitoa kila kitu. Walishambulia vizuri, tulikosa makali eneo la mwisho. Mlinda mlango wao Philipp Kohn aliokoa vyema. Waliweka vizuizi vingi na hatukuwa vizuri kwenye kumalizia kila wakati. Inabidi tujitoe mavumbi, lakini tutakuwa bora zaidi. Nimesikitishwa na matokeo lakini wachezaji wangu walitoa kila kitu lakini haikuwa siku yetu.’’ Amesema Graham Potter

Potter alitangazwa kuwa kocha wa Chelsea siku 6 zilizopita akichukua mikoba ya kocha Thomas Tuchel aliyefutwa kazi wiki iliyopita. Kwa matokeo ya sare Chelsea imefikisha alama 1 katika michezo 2 ya kundi E wakiwa nyuma kwa tofauti ya alama 3 dhidi ya vinara wa kundi hilo AC Milan wenye alama 4.


Post a Comment

0 Comments