Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yaelekeza nguvu Ligi ya Mabingwa Afrika

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC utakaofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

KATIKA mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Zalan wakiwa wenyeji, Yanga ilishinda mabao 4-0 na hivyo kutanguliza mguu mmoja katika mchezo wa pili wa hatua hiyo ya awali.

Nabi alisema mbali na kuelekeza nguvu katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, pia watakuwa wakiangalia hali ya wachezaji wake, akiwemo waliopata majeraha, Khalid Aucho na Jesus Moloko kama watakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza Jumamosi. Alisema wachezaji wake walicheza vizuri licha ya ugumu na uhodari wa Mtibwa na kufanikiwa kuondoka na mabao hayo matatu na pointi hizo tatu.

“Nawapongeza Mtibwa Sugar kwa mchezo mzuri waliocheza, mechi ilikuwa nzuri kwa pande zote mbili kipindi cha kwanza tulifanya vizuri tukapata matokeo kipindi cha pili nilifanya mabadiliko ya kuongeza baadhi ya wachezaji kuongeza nguvu.” “Kipindi cha pili wachezaji walionekana wamechoka hivyo ikabidi baadhi wapumzike na wengine waingie japokuwa sikupata matokeo niliyotarajia, lengo langu lilikuwa kuwapumzisha ili wengine wapate nafasi,” alisema Nabi.

Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Salum, alisema anashukuru Mungu kwa kumaliza mchezo salama japokuwa wamepoteza kwa mabao 3-0.

“Kwa jinsi walivyocheza Yanga walistahili kupata pointi tatu, tunawapongeza lakini ligi bado inaendelea, tunaenda kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

Post a Comment

0 Comments